Johabes Lugenge kushoto na Lucas Rutainurwa |
WAANDAAJI wa
pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gariwatakalogombania Mabondia Mada Maugo Na Francis |
Cheka Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA,
Dar
es Salaam.
Pambano hilo
linatarajiwa kuwa katika uzito wa
kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo
linatarajiwa
kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Tanzania
(TPBC) huku majaji wa pambano
hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza
Dar es Salaam leo, Msemaji wa
mpambano huo Yasini Abdallah amesema
kuanikwa kwa
mkanda huo na Gari kuwekwa
Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano
hilo
ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa
ili kuweza kupatikana kwa
mshindi wa halali na pia litafuta
hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano
hilo.
kaike
amesema kuwa wameamua kuanika
Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa
ngumi
na mashabiki kwa ujumla kuwa wapo
makini
na pambano hilo na sio la kibabaishaji na
kama walivyosema hapo awali kuwa
majaji watoka
nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe
kulingana na
hadhi ya mkanda
Amesema,
maandalizi kwa ujumla ya pambano
hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa
mshindi liko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa
siku hyio hyio ya pambanomra
tu baaday ya
kutangazwa mshindi na kupewa
mkanda
itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali
mabondia hao walishakutana mara
mbili ulingoni ambapo katika pambano la
kwanza
lilofanika PTA Cheka alishinda kwa
pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo
hao
na kuandaliwa pambano la marudiano
lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro
ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa
kumtwanga kwa pointi.
Baada ya
kumalizika kwa pambano hilo kila
bondia aligoma kucheza na mwenzake tena
lakini
baada ya kuandaliwa pambano hilo la
ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na
kuamua
kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
No comments:
Post a Comment