Sunday, April 22, 2012

NIZAR ATUA SIMBA







KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa
 anacheza soka ya kulipwa Marekani, amejiunga rasmi na
 `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu
 huu, Simba.
Habari za kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo zimeenea
 zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa
 na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo,
 Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo, alikiri na
 kusema kuwa, aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha
 usajili wa mchezaji huyo na kwamba baada ya kufanikiwa
, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu.
“Kama Mwanasimba, nimetimiza wajibu wangu kama
 nilivyokuwa nimeombwa na uongozi. Nimeambiwa
 ataungana na wenzake kuanza mazoezi wakati wowote
 kuanzia Jumatatu (leo),” alisema na kuongeza kuwa,
 mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na
 Moro United atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea 
Simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu endapo
 itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Baada ya kuzing’oa ya Kiyovu ya Rwanda na Setif ya
 Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya
 Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho
, itaingia katika raundi nyingine itakayoamua timu
 za kucheza Nane Bora Afrika.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nizar leo
 atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa 
Simba. Atakabidhiwa jezi hiyo siku moja kabla ya
 mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Moro United
 unaotarajiwa kuanza saa kumi alasiri.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hata
 hivyo hakuwa tayari kutajwa jina akisema si
 msemaji, alikiri kukamilika kwa taratibu za Nizar
 kutua Simba huku akiongeza kuwa, ataisaidia
 klabu hiyo katika michuano ya ligi na ile ya
 kimataifa kuanzia msimu ujao.
“Ni kweli, timu inazidi kuimarika. Kumpata staa
 wa kimataifa kama Nizar ni jambo la kujivunia,
 tunashukuru kwa juhudi zilizofanyika na hatimaye
 kumpata mchezaji huyu,” alisema.
Nizar ambaye Juni 21 mwaka huu atatimiza
 umri wa miaka 24, kabla ya kutua Simba 
aliichezea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya
 Marekani aliyodumu nayo kwa miezi mitatu tu
 baada ya kujiunga nayo akitokea Vancouver
 Whitecaps. Alikuwa Vancouver tangu Agosti
 22, mwaka 2009 akitokea Moro United.
Katika soka ya ushindani, nyota huyo aliibuki
a timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
 miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004 na
 baadaye akajiunga na Mtibwa Sugar kabla ya
 kutimkia Kuwait kuichezea Al Tadamon ya
 huko msimu wa 2007-2008. Kutoka Tadamon
 alikwenda Lebanon na kuichezea Tadamon Sour
 ya huko na mwaka 2009 aliichezea Moro United.

No comments:

Post a Comment