Mchezaji mpya wa mabingwa wa tarajiwa wa Tanzania Bara Simba SC, Nizar Khalfan hakuweza kutambulishwa katika mchezo wa leo kama ilivyotangazwa hapo awali.
Akizungumza baada ya ushindi wa goli 3-0
walioupata leo, ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kuwa zoezi la utambulisho lilishindikana baada ya Nizar Khalfan kuuguliwa na mamaake, hivyo kushindwa kufika katika uwanja wa Taifa.
Kamwaga alisema kuwa watapanga siku nyingine
ya kumtambulisha kiungo huyo anayesifika kwa kupiga mashuti ya mbali, baada ya kushindikana leo.
Nizar amesajiliwa Simba SC kwa
ajili ya michezo ya kimataifa kama watatinga hatua ya nane bora ya kombe la shirikisho CAF, na michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kurindima kati ya mwezi wa 6 ama wa 7 na msimu ujao. |
No comments:
Post a Comment