MECHI ZA VPL WIKIENDI HII, MAREKEBISHO
Ligi Kuu ya Vodacom
inaingia raundi ya 24 wikiendi hii kwa mechi mbili zitakazochezwa Aprili 22
jijini Dar es Salaam. Villa Squad itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa
Chamazi wakati Yanga itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma katika Uwanja wa
Taifa.
Azam na Mtibwa Sugar zilizokuwa zicheze Aprili 21 mwaka huu sasa
zitacheza Aprili 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati
siku hiyo hiyo jioni kutakuwa na mechi kati ya Simba na Moro United. Mechi zote
zitaanza saa 10.30 jioni.
Oljoro JKT itaikaribisha
Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha
wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar
es Salaam.
Raundi ya 25 itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28 mwaka huu
Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam na Toto African zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka
huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi
hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa
uwanjani.
Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa),
Oljoro JKT vs Polisi Dodoma
(Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha)
Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini,
Mlandizi)
Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga)
African Lyon vs
JKT Ruvu (Manungu, Morogoro)
Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es
Salaam)
Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).
No comments:
Post a Comment