Tuesday, April 24, 2012

MAKUSANYOKATIKA MICHEZO YA VPLNA NGORONGORO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi 

wanne wa Tanzania kuchezesha mechi ya marudiano ya 16

 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Black Leopards

 ya Afrika Kusini na Warri Wolves ya Nigeria itakayochezwa

 nchini Afrika Kusini kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.


Waamuzi hao ni Waziri Sheha atakayepuliza filimbi

 wakati wasaidizi wake watakuwa John Kanyenye

 na Erasmo Jesse. Mwamuzi wa akiba

 (fourth official) atakuwa Israel Mujuni.

 Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Aurelio

 Mathias wa Msumbiji.


Mechi ya kwanza kati ya timu hizo itachezwa Jumapili

 (Aprili 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa

 Warri City ulioko Jimbo la Delta nchini Nigeria na

 itachezeshwa na waamuzi kutoka Senegal wakati

 Kamishna atakuwa Inyangi Bokinda wa Jamhuri

 ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).


1,635 WASHUHUDIA MECHI YA YANGA, POLISI DODOMA


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Polisi

 Dodoma iliyochezwa (Aprili 22 mwaka huu)

 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

 ilishuhudiwa

 na watazamaji 1,635 na kuingiza sh. 5,666,000.


Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na

 asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

 ambayo ni sh. 864,305.08 kila klabu ilipata

 sh. 193,858.47, uwanja sh. 26,469.49. Shirikisho

 la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 26,469.49, 

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa 

Dar es Salaam (DRFA) sh. 108,687.80.

 Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu

 (FDF) sh. 13,234.75, Baraza la Michezo la Taifa

 (BMT) sh. 2,646.95 na asilimia 10 ya gharama

 za mechi ni sh. 26,469.49.


Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani

 kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa

 kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa

 akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna

 na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 1,500,000

, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 1,500,000 na Wachina

 (Beijing Construction) sh. 1,000,000.


Kutokana na mechi hiyo kuingiza kiasi kidogo baadhi ya

 gharama zililipwa nusu au kutolipwa kabisa na kuacha

 madeni. Madeni hayo ni tiketi sh. 1,500,000, 

maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000,

 umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja

 sh. 850,000 na Wachina sh. 1,000,000.


POLISI MORO, MGAMBO, PRISONS ZAPANDA VPL


Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyoshirikisha

 timu tisa imemalizika jana (Aprili 23 mwaka huu)

 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini

 Morogoro huku tatu zikifuzu kucheza Ligi

 Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2012/2013

 utakaonza Agosti mwaka huu.


Timu hizo ni Polisi Morogoro iliyofikisha pointi 

20 ikifuatiwa na Mgambo Shooting ya

 Tanga (15) na Tanzania Prisons ya Mbeya

 iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14.


Nyingine zilizofuatia na pointi zao kwenye

 mabano ni Polisi Dar es Salaam (13),

 Mbeya City Council (11), Rhino Rangers ya Tabora (8),

 Mlale JKT ya Ruvuma (8), Polisi Tabora (6) na

 Transit Camp ya Dar es Salaam (2).


SIMBA, MORO UNITED ZAINGIZA MIL 28/-


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na

 Moro United lililochezwa jana (Aprili 23 mwaka huu)

 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 28,688,000.


Jumla ya watazamaji 7,945 walikata tiketi kushuhudia

 mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000,

 sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 6,946 kati ya

 hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.


Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na

 asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

 ambayo ni sh. 4,376,135.59 kila klabu

 ilipata sh. 4,919,009.32, uwanja sh. 1,454,286.44.

 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.

 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa Miguu

 Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,058,414.58,

 Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)

 sh. 727,143.22, Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

 sh. 145,428.64

 na asilimia 10 ya gharama za 

mechi ni sh. 1,454,286.44.


Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya

 ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani

 kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000, mwamuzi

 wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa

 kamishna na waamuzi sh. 80,000, gharama

 ya tiketi sh. 3,000,000, maandalizi ya

 uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000,

 usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na

 Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.


Nayo mechi kati ya Villa Squad na African Lyon

 iliyochezwa Aprili 22 mwaka huu kwenye

 Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam 

iliingiza sh. 496,000 ambapo kila klabu ilipata

 sh. 68,061.70 wakati watazamaji

 walioshuhudia mechi hiyo ni 469.


Vilevile mechi kati ya

Tanzania (Ngorongoro Heroes) na

 Sudan iliyochezwa Aprili 21 mwaka huu

 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

iliingiza sh. 9,717,000 kutokana na

 washabiki 2,562.

No comments:

Post a Comment