Tuesday, April 24, 2012


Ligi Kuu ya Vodacom imeingia raundi ya 25 ambapo 
kesho (Aprili 25 mwaka huu) Oljoro JKT itaikaribisha
 Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
 Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT
 Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye
 Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Raundi hiyo itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28
 mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa
 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani
 jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa
 African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.

Azam na Toto African zitacheza Chamazi,
 Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka
 huu Villa Squad itaumana na
 Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.

Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012,
 Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote
 14 zitakuwa uwanjani.

Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa),
 Oljoro JKT vs Polisi Dodoma
 (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha)
 na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).

Mechi nyingine zitakuwa kati ya
 Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), 
African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu,
Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam)
 na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).

MAKUSANYOKATIKA MICHEZO YA VPLNA NGORONGORO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi 

wanne wa Tanzania kuchezesha mechi ya marudiano ya 16

 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Black Leopards

 ya Afrika Kusini na Warri Wolves ya Nigeria itakayochezwa

 nchini Afrika Kusini kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.


Waamuzi hao ni Waziri Sheha atakayepuliza filimbi

 wakati wasaidizi wake watakuwa John Kanyenye

 na Erasmo Jesse. Mwamuzi wa akiba

 (fourth official) atakuwa Israel Mujuni.

 Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Aurelio

 Mathias wa Msumbiji.


Mechi ya kwanza kati ya timu hizo itachezwa Jumapili

 (Aprili 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa

 Warri City ulioko Jimbo la Delta nchini Nigeria na

 itachezeshwa na waamuzi kutoka Senegal wakati

 Kamishna atakuwa Inyangi Bokinda wa Jamhuri

 ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).


1,635 WASHUHUDIA MECHI YA YANGA, POLISI DODOMA


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Polisi

 Dodoma iliyochezwa (Aprili 22 mwaka huu)

 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

 ilishuhudiwa

 na watazamaji 1,635 na kuingiza sh. 5,666,000.


Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na

 asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

 ambayo ni sh. 864,305.08 kila klabu ilipata

 sh. 193,858.47, uwanja sh. 26,469.49. Shirikisho

 la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 26,469.49, 

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa 

Dar es Salaam (DRFA) sh. 108,687.80.

 Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu

 (FDF) sh. 13,234.75, Baraza la Michezo la Taifa

 (BMT) sh. 2,646.95 na asilimia 10 ya gharama

 za mechi ni sh. 26,469.49.


Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani

 kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa

 kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa

 akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna

 na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 1,500,000

, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 1,500,000 na Wachina

 (Beijing Construction) sh. 1,000,000.


Kutokana na mechi hiyo kuingiza kiasi kidogo baadhi ya

 gharama zililipwa nusu au kutolipwa kabisa na kuacha

 madeni. Madeni hayo ni tiketi sh. 1,500,000, 

maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000,

 umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja

 sh. 850,000 na Wachina sh. 1,000,000.


POLISI MORO, MGAMBO, PRISONS ZAPANDA VPL


Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyoshirikisha

 timu tisa imemalizika jana (Aprili 23 mwaka huu)

 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini

 Morogoro huku tatu zikifuzu kucheza Ligi

 Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2012/2013

 utakaonza Agosti mwaka huu.


Timu hizo ni Polisi Morogoro iliyofikisha pointi 

20 ikifuatiwa na Mgambo Shooting ya

 Tanga (15) na Tanzania Prisons ya Mbeya

 iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14.


Nyingine zilizofuatia na pointi zao kwenye

 mabano ni Polisi Dar es Salaam (13),

 Mbeya City Council (11), Rhino Rangers ya Tabora (8),

 Mlale JKT ya Ruvuma (8), Polisi Tabora (6) na

 Transit Camp ya Dar es Salaam (2).


SIMBA, MORO UNITED ZAINGIZA MIL 28/-


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na

 Moro United lililochezwa jana (Aprili 23 mwaka huu)

 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 28,688,000.


Jumla ya watazamaji 7,945 walikata tiketi kushuhudia

 mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000,

 sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 6,946 kati ya

 hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.


Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na

 asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

 ambayo ni sh. 4,376,135.59 kila klabu

 ilipata sh. 4,919,009.32, uwanja sh. 1,454,286.44.

 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.

 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa Miguu

 Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,058,414.58,

 Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)

 sh. 727,143.22, Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

 sh. 145,428.64

 na asilimia 10 ya gharama za 

mechi ni sh. 1,454,286.44.


Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya

 ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani

 kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000, mwamuzi

 wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa

 kamishna na waamuzi sh. 80,000, gharama

 ya tiketi sh. 3,000,000, maandalizi ya

 uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000,

 usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na

 Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.


Nayo mechi kati ya Villa Squad na African Lyon

 iliyochezwa Aprili 22 mwaka huu kwenye

 Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam 

iliingiza sh. 496,000 ambapo kila klabu ilipata

 sh. 68,061.70 wakati watazamaji

 walioshuhudia mechi hiyo ni 469.


Vilevile mechi kati ya

Tanzania (Ngorongoro Heroes) na

 Sudan iliyochezwa Aprili 21 mwaka huu

 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

iliingiza sh. 9,717,000 kutokana na

 washabiki 2,562.


BINGWA wa kick Boxing. Japhet Kaseba amesaini

 mkataba wa

 kucheza na Bingwa wa dunia wa ndondi 

mkanda unaomilikiwa

 na IBC, Francis Cheka wa Morogoro

 katika uzani wa 

KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba

 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba

 huo Kaseba

 amesema anashukulu kupata

 mpambano huo na

 atahakikisha anaonesha uwezo

 wake wote

 katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa

 wa mapambano;

"Najua mabondia wa hapa bongo

 wananikwep

a sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa

 wa ngumi 

za mateke lakini awajui mimi ni 

bingwa katika

 mapigano yote," alisema Kaseba.

"Nitahakikisha naweka kambi

 ya kutosha

 na kukata

 ngebe za cheka ni mtoto mdogo

 sana katika

 masumbwi kwa kweli bingwa wa

 kweli n

i Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu

 mpaka

 sasa Cheka kanikimbia mda mrefu tu

 tangia

 tupambane 3 October 2009 ambapo

 alipewa 

ubingwa kwa kusingizia mshabiki 

wangu, alikuja

 kumtupa nje ya uwanja kazi yake yeye

 anarudiana

 na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa

 kakanyaga miwaya zamu yake imefika."

Nae Promota wa mpambano huo Kaike

 Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika

 Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni

 mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa

 mabondia hao wanakubalika na mashabiki

 wa ndani na nje ya Nchi.

Mbali na mpambano huo pia kutakua na

 mapambano ya utangulizi na burudani 

mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae.

NIZAR ASHINDWA KUTAMBULISHWA RASMI

 

Mchezaji mpya wa mabingwa wa tarajiwa wa

 Tanzania Bara Simba SC, Nizar Khalfan

 hakuweza kutambulishwa katika mchezo

 wa leo kama ilivyotangazwa hapo awali.


Akizungumza baada ya ushindi wa goli 3-0 

walioupata leo, ofisa habari wa Simba Ezekiel

 Kamwaga alisema kuwa zoezi la utambulisho 

lilishindikana baada ya Nizar Khalfan 

kuuguliwa na mamaake, hivyo kushindwa

 kufika katika uwanja wa Taifa.


Kamwaga alisema kuwa watapanga siku nyingine

 ya kumtambulisha kiungo huyo anayesifika kwa

 kupiga mashuti ya mbali, baada ya kushindikana leo.


Nizar amesajiliwa Simba SC kwa

 ajili ya michezo ya 

kimataifa kama watatinga hatua ya nane bora

 ya kombe la shirikisho CAF, na michuano

 ya Kagame Cup inayotarajiwa kurindima 

kati ya mwezi wa 6 ama wa 7 na msimu ujao.

Monday, April 23, 2012

ROBIN VAN PERSIE AN'GARA



Robin Van Persie atwaa tuzo ya mwanasoka bora wa kulipwaNaye beki
wa kulia wa Totenham Hotspurs Kyle Walker alichaguliwa mwanasoka
bora kijana akiwashinda Sergio Aguero na Danny Welbeck.

Premier League team of the year:

Joe Hart (Man City), Kyle Walker (Tottenham), Vincent Kompany (Man City),
Fabricio Coloccini (Newcastle), Leighton Baines (Everton)
, David Silva (Man City), Yaya Toure (Man City), Gareth Bale (Tottenham),
Scott Parker (Tottenham), Robin van Persie (Arsenal), Wayne Rooney (Man Utd).

Championship team:

Kelvin Davis (Southampton), Nathaniel Clyne (Crystal Palace)
, James Tomkins (West Ham), Curtis Davies (Birmingham),
Ian Harte (Reading), Adam Lallana (Southampton),
Peter Whittingham (Cardiff), Mark Noble (West Ham),
Matt Phillips (Blackpool), Rickie Lambert (Southampton), 
Jay Rodriguez (Burnley).

MNYAMA ATWAA UBINGWA

Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa kwa

ngazi klabu, Simba SC wametwawazwa Ubingwa wa

 Tanzania Bara baada ya Kushinda goli 3-0,

huku wapinzani wake katika mbio hizo Azam FC

wakitoka sare ya goli 1-1.

 Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom

 Simba SC waliandika goli la kwanza kupitia

 kwa Patrick Mafisango, huku Haruna Moshi

Boban akiiandikia goli la pili.

 Simba walihitimisha goli la 3 kupitia kwa

 Felixs Sunzu, na mpaka kipenga cha mwisho

Simba SC 3-0 Moro united

 Katika mchezo mwingine uliochezwa

Chamanzi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar

 ulivunjika baada ya Mtibwa Sugar walio kuwa

pungufu kugomea penati ya Azam FC katika

 dakika za majeruhi.

 Mchezo huo ulivunjika matokeo ya kiwa goli 1-1,

yaliyofungwa na Salum Swedi kwa upande wa

Mtibwa na Mrisho Ngassa kwa upande

        wa Azam FC


ZAWADI YA PAMBANO LA CHEKA NA MAUGO HADHARANI



 Johabes Lugenge kushoto na Lucas Rutainurwa   

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis
Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi
 gariwatakalogombania  Mabondia
Mada Maugo Na Francis
Cheka  Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA,
Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa
kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa
kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano
hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa
mpambano huo Yasini Abdallah amesema
kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa
Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano
hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa
ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia litafuta
hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
kaike amesema kuwa wameamua kuanika
Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa
ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa wapo
 makini na pambano hilo na sio la kibabaishaji na
kama walivyosema hapo awali kuwa majaji watoka
nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe
kulingana na hadhi ya mkanda
Amesema, maandalizi kwa ujumla ya pambano
hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa
mshindi liko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa
siku hyio hyio ya pambanomra tu  baaday ya
kutangazwa mshindi na kupewa mkanda
itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara
mbili ulingoni ambapo katika pambano la
kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa
pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo
hao na kuandaliwa pambano la marudiano
lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro
ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa
kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila
bondia aligoma kucheza na mwenzake tena
lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la
ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua
kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.

Sunday, April 22, 2012

NIZAR ATUA SIMBA







KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa
 anacheza soka ya kulipwa Marekani, amejiunga rasmi na
 `Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu
 huu, Simba.
Habari za kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo zimeenea
 zinasema kuwa, usajili wa mchezaji huyo umefanikishwa
 na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo,
 Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo, alikiri na
 kusema kuwa, aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha
 usajili wa mchezaji huyo na kwamba baada ya kufanikiwa
, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu.
“Kama Mwanasimba, nimetimiza wajibu wangu kama
 nilivyokuwa nimeombwa na uongozi. Nimeambiwa
 ataungana na wenzake kuanza mazoezi wakati wowote
 kuanzia Jumatatu (leo),” alisema na kuongeza kuwa,
 mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na
 Moro United atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea 
Simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu endapo
 itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Baada ya kuzing’oa ya Kiyovu ya Rwanda na Setif ya
 Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya
 Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho
, itaingia katika raundi nyingine itakayoamua timu
 za kucheza Nane Bora Afrika.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nizar leo
 atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa 
Simba. Atakabidhiwa jezi hiyo siku moja kabla ya
 mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Moro United
 unaotarajiwa kuanza saa kumi alasiri.
Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hata
 hivyo hakuwa tayari kutajwa jina akisema si
 msemaji, alikiri kukamilika kwa taratibu za Nizar
 kutua Simba huku akiongeza kuwa, ataisaidia
 klabu hiyo katika michuano ya ligi na ile ya
 kimataifa kuanzia msimu ujao.
“Ni kweli, timu inazidi kuimarika. Kumpata staa
 wa kimataifa kama Nizar ni jambo la kujivunia,
 tunashukuru kwa juhudi zilizofanyika na hatimaye
 kumpata mchezaji huyu,” alisema.
Nizar ambaye Juni 21 mwaka huu atatimiza
 umri wa miaka 24, kabla ya kutua Simba 
aliichezea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya
 Marekani aliyodumu nayo kwa miezi mitatu tu
 baada ya kujiunga nayo akitokea Vancouver
 Whitecaps. Alikuwa Vancouver tangu Agosti
 22, mwaka 2009 akitokea Moro United.
Katika soka ya ushindani, nyota huyo aliibuki
a timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
 miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004 na
 baadaye akajiunga na Mtibwa Sugar kabla ya
 kutimkia Kuwait kuichezea Al Tadamon ya
 huko msimu wa 2007-2008. Kutoka Tadamon
 alikwenda Lebanon na kuichezea Tadamon Sour
 ya huko na mwaka 2009 aliichezea Moro United.

Saturday, April 21, 2012

BARCA CHALIIIII



Ulimwengu mzima umeshuhudia Barca wakilala kwa goli 2

 kwa 1 katika El Clasico na mahasimu wao vijana wa

 kocha msema hovyo Mreno Jose Morinho aka special one

Real walikuwa wakwanza kuliona lango la mahasimu wao

 kwa goli safi la dakika ya 17 mara baada ya Sami Khedira

 kutikisa nyavu za Wakalunya hao

Dakika ya 70 Alexis Sanchez alisawazisha goli hilo lakini

mambo yakawa mabaya mnamo dakika ya 72 Mreno

 Christiano Ronaldo alipoifungia Real goli la ushindi

Friday, April 20, 2012

MECHI ZA VPL WIKIENDI HII, MAREKEBISHO

Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 24 wikiendi hii kwa mechi mbili zitakazochezwa Aprili 22 jijini Dar es Salaam. Villa Squad itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Yanga itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma katika Uwanja wa Taifa.


Azam na Mtibwa Sugar zilizokuwa zicheze Aprili 21 mwaka huu sasa zitacheza Aprili 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati siku hiyo hiyo jioni kutakuwa na mechi kati ya Simba na Moro United. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.

Oljoro JKT itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.


Raundi ya 25 itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28 mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi. Azam na Toto African zitacheza Chamazi, Aprili 30 mwaka huu wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.


Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani.

Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa),

Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha)

Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi)

Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga)

African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro)

Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam)

Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).


MALINZI MGENI RASMI MKUTANO MKUU TFF

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.


Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini leo (Aprili 20 mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.


Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited accounts).


KOCHA NGORONGORO HEROES AAHIDI USHINDI

Kocha Kim Poulsen anayeinoa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 cha Tanzania (Ngorongoro Heroes) ameahidi kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Sudan.

Akizungumza leo (Aprili 20 mwaka huu) kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, Poulsen amesema timu yake imejiandaa vizuri kwa mechi hiyo na kiu yao ni kushinda.

Kwa upande wake Kocha wa Sudan, Azhari Osman El Tahir amesema ingawa haifahamu vizuri timu ya Tanzania, lakini wamejiandaa kushinda kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajashiriki mashindano ya vijana ya kimataifa.

Mechi hiyo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa kesho (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000.

Sudan iliwasili nchini jana (Aprili 19 mwaka huu) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, viongozi kumi na mwandishi wa habari mmoja kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza kabla ya timu hizo kurudiana jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.

Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Brian Miiro atakayesaidiwa na Mark Ssonko, Lee Patabali na Denis Batte wote kutoka Uganda. Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo namba 15.

Fainali za Afrika kwa michuano hiyo zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria wakati za Dunia zitafanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai mwakani. Katika fainali za Dunia, Afrika itawakilishwa na timu nne za kwanza kwenye fainali za Algeria.


Wednesday, April 18, 2012

CHELSEA KULIPA KISASI???

Vigogo viwili wa soka huko ulaya kukipiga leo ili kumtsfuta 

mbabe ambaye atakipiga na timu itakayofudhu kucheza

 fainali za ligi ya mabingwa kati ya vijana wa kocha 

msema hovyo Morinho na Beyern munich. katika mchezo

 wa leo Chelsea watakuwepo katika uwanja wao wa nyumbani

Stanford bridge kukipiga na Barcelona. . Iumbukwe ya kwamba

 mwaka 2009 Barca waliitoa The Blues katika nusu fainali

Monday, April 16, 2012

FABIO KUONDOKA UNITED KWA MKOPO

Beki wa Manchester United Mbrazil Fabio Da Silva 

ataondoka katika kikosi cha Mashetani wekundu

 mwishoni mwa msimu huu kwa mkopo.Kibabu

 Fergie amesema kwamba anaamini kuwa Fabio 

anahitaji kucheza katika kikosi cha kwanza

 ili kupata uzoefu zaidi. .  . Kwa upande wake 

Fabio amekubaliana na wazo hilo

Sunday, April 15, 2012

ALIKAIBA AKANUSHA KUMCHUKUA LULU SIKU YA KIFO CHA KANUMBA




Mshindi wa wimbo bora wa zouk rhumba katika tuzo

za Kilimanjaro Tanzania Music Awards mtu mzima

Ali Kiba amekanusha kwamba usiku aliofariki Kanumba

yeye ndo alienda kumchukua Lulu, Wakati tukio linatokea

 Ali Kiba alikuwa kiwanja cha coco beach ndipo

kwamba Kanumba kafariki, Ndipo akampigia simu Lulu

kumuliza kama ni kweli Kanumba kafariki Lulu alimwambia

 hapana hajafa anaumwa tu.

 Muda si mrefu akapokea

simu kutoka kwa mama mtoto wake anaekaa Sinza

akamwambia ni kweli ameona mwili wake ukiingizwa

 mochwari. Ali Kiba asubuhi yake alisafiri kueleka

Malindi/Mombasa Kenya

 

HAWA NDO WASHINDI WA KILI MUSIC AWARDS 2012.

 

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-

7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-

9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).

11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-

12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-

15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-
16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-

17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-

18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-

19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
      - BARNABA-

RADIO 5 YAKABIDHI ZAWADI YA MIPIRA TOKA BBC KWA WASHINDI



Program Manager wa radio 5 Prince Baina Kamukulu akimkabidhi

 mpira Jacob

Paulo mpira toka  BBC mara baada ya kushinda. Kwa

 nyuma ni Willy Protas

Cosmas Mhariri Mkuu wa sports Radio 5



mkazi wa Arusha Ibraheem Rashid nae aliibuka kidedea na kujishindia

 mpira toka BBC

Yohane Chance akikabidhiwa  mpira


Yohane, Jacob na Ibraheem wakionesha zawadi zao

Saturday, April 14, 2012

"GANGSTA" PINI KALI KUTOKA NOIZ MEKAZ

Pini hili la  "Gangsta",ni collabo kati ya hiphop 

Mc's anzia Dar-Arusha-Mombasa mpaka 

Nairobi.Artists walopita ni BouNako, FiDo, 

MoPlus, Frost ,GeeZMabov, LavosT na 

RitchieRich,Hiphop ni worldwide na 

tunafanya kazi kwa pamoja kuimarisha 

\game na mshikamano ambao upo kati 

yetu wasanii,Geez Mabov anarepresent Dirty 

South pande za DSM,FiDo,MoPlus,Frost

 na BouNako wanarepresent Arachuga,Lavosti

 toka Ukoo MauMau anarepresent Mombasa

 na RitchieRich toka HeadBangaz International 

akirepresent pale Nairobi City,Audio ikiwa 

imesmamiwa pande za Noizmekah Studios,

Video ya pini hili inaendelezwa editing Pande 

za RED Films Arusha..

SIZ KITAA SEASON YA TATU KUANZA JUMATATU

MABADILIKO:
  1. MUDA NI SAA 1:00-1:30 ZA JIONI BADALA YA SAA 1:15-1:45
 ZA JIONI KAMA ILIVYOKUWA IMEZOELEKA.
         2. MASKANI YA CASTO DICKSON MWANANCHI WA KAWAIDA KWA
AJILI  YA SIZ KITAA SEASON 3.


Hii ndio logo mpya itakayoonekana kwenye kipindi kipya cha Siz Kitaa
Na hapa ndipo maskani penyewe kiroho safiiii shughuli zote zitapigwa hapa

Thursday, April 12, 2012

BABA WA MSANII LULU AFUNGUKA

Baba wa msanii Elizabeth michael ambaye yupo Rombo mkoani Kilanjaro  awataka watanzania kuacha ushabiki kuhusiana na kesi inayomkabili binti yake kuhusiana na kuhusika na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven charles kanumba na kuwataka watanzania waiache mahakama itende haki 

Tuesday, April 10, 2012

MADAKTARI WAELEZA KILICHOMUUA KANUMBA


MADAKTARI WAELEZA KILICHOMUUA KANUMBA

THE LATE KANUMBA



Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo

UMATI WA WATU WAFIKA MAKABURI YA KINONDONI

WAOMBOLEAJI WAKIWA WENYE HUZUNI. CHINI NI

MKAZI AMBAYE AMEZIMIA



POLISI WALISHINDWA KUFANYA KAZI KWANI WATU 

WALIKUWA WENGI SANA


WATU WALIKUWA WENGI SANA

JENEZA LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU STEVEN

 KANUMBA LIKISOGEZWA KARIBU NA KABURI


WAZIRI MKUU MH MIZENGO PINDA AKITETA JAMBO


ILIWALAZIMU WATU KUPANDA JUU YA MITI ILI

 KUSHUHUDIA KINACHOENDELEA


MAKAMU WA RAISI AONGOZA WAOMBOLEZAJI LEARDEZ

WANAKWAYA WAKIIMBA NYIMBO ZA MAOMBOLEZO

MAMA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

MWILI WA MAREHEMU UKIWASILI LEARDEZ
       WAFANYAKAZI WA MSALABA MWEKUNDU WAKIMBEBA
 MUOMBOLEZAJI ALIYEZIMIA

VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI WAKIWASILI

MKE WA RAISI MAMA SALMA KIKWETE AKIWASILI

DADA WA STEVEN KANUMBA AKIBEBWA MARA BAADA YA
 KUISHIWA NGUVU
MDOGO WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA AKIWASILI LEARDEZ